WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA KAMATI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YA KUSHUGHULIKIA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/01/aziri-makamba-akutana-na-kamati-ya_25.html
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambao pia ni wajumbe wa kamati ya Kusimamia viongozi wakuu wa kitaifa wamekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Muungano na Mazingira Mh. January Makamba, Jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo la kuzungumzia baadhi ya changamoto za Muungano na kubadilishana mawazo katika maeneo ya Muungano.
Waziri Makamba aliwapongeza wajumbe wa Kamati hiyo, na kusema kuwa ujio wao unaonyesha dhamira nzuri ya kuwawakilisha wananchi wa Zanzibar na kuimarisha Muungano uliodumu kwa miaka hamsini na saba (53) sasa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Omary Seif Abeid ambaye pia ni Muwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba, alisema kuwa, pande hizi mbili za Muungano hazina Budi kuwakumbuka waasisi wa Muungano huo Hayati Mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuunganisha pande mbili hizi na kupatikana kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kuwa anaeubeza Muungano anajibeza mwenyewe.

