nike kumzawadia rooney kiatu kwakuvunja rekod ya kupachika mabao klabuni hapo

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/01/nike-kumzawadia-rooney-kiatu-kwakuvunja.html
Rooney Jumamosi alifunga bao dakika za majeruhi kuisaidia Manchester United kuchomoka kwenye kipigo kutoka kwa Stoke City, lakini bao hilo limebadili kila kitu katika historia yake ya kisoka na kuwafanya kampuni ya Nike kumtengenezea viatu maalumu vya soka.
Bao hilo lilikuwa la 250 klabuni Man United na hivyo kumfanya Rooney kuwa kinara wa mabao katika historia ya timu hiyo jambo lililoifanya Nike kuthamini rekodi yake hiyo na kumtengenezea viatu maalumu kwa ajili yake itakavyoitwa Hypervenom WR250.
Rekodi ya mabao kwa miaka mingi ilikuwa ikishikiliwa na Sir Bobby Charlton, lakini sasa Rooney ameivunja na hivyo kuwa gwiji rasmi la Old Trafford. Kiatu hicho kipya cha Rooney kitakuwa na rangi nyekundu na nyeupe, ambazo supastaa huyo amekuwa akizivaa katika klabu yake na timu ya taifa ya England.
Kiatu hicho kwenye ulimi wake kuna maneno WR250, wakati pembeni kuna maneno WR10, ikiwa na maana ya jezi namba anayovaa staa huyo.
Rooney ana mradi wake unaoshughulikia watoto na alisema: “Nataka kufanya mambo mazuri si kwa watoto wangu, bali watoto wote,” aliongeza Rooney, ambaye ni baba wa watoto watatu wa kiume, Kai, Klay na Kit. “Na ndio maana nimeanzisha Wayne Rooney Foundation. Kila bao ninalofunga, nimefunga nikiwa na kiatu cha Nike, hivyo kuna kitu kinafanyika kwenye mradi wangu, sio suala la rekodi tu.”