vijana wa CCM vitani na wasiotekeleza ahadi zao.

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/01/vijana-wa-ccm-vitani-na-wasiotekeleza.html
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani ileje, John Mwakifuna amesema chama hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na baadhi ya viongozi wake kutotekeleza kuto wajibika ipasavyo kwa wananchi wao.
Mwakifuna alisema hayo mwishoni mwa wiki kwenye kikao na Mwenyekiti wa UVCCM wa mikoa ya Songwe na Mbeya, Aman Kajuna aliyetembelea wilayani hapa kukagua miradi ya vijana.
“Tunapata wakati mgumu kwa wapiga kura na kuhojiwa maswali magumu kutokana na wagombea waliopita katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutotekeleza ahadi na hasa zinazohusu kuboresha miundombinu ya barabara, zahanati kila kijiji na pembejeo za kilimo kutofika kwa wakati,” .
Alisema baadhi ya wenyeviti wa vijiji, madiwani na wabunge hawawatembelei wananchi kujua kero zao na kuzitafutia majawabu.