Aveva atia nguvu Simba Zanzibar

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/02/aveva-atia-nguvu-simba-zanzibar.html

Rais wa klabu ya SimbaEvance Aveva
Katika kuhakikisha Simba inapata ushindi Jumamosi dhidi ya Yanga, rais wa klabu hiyo Evance Aveva alionekana katika mazoezi ya timu hiyo asubuhi.
Simba imeweka kambi yake visiwani Zanzibar kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.
Aveva aliyeshuhudia mazoezi ya Simba amesema, ameamua kiongozana na timu ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
"Unapokuwa karibu kila kitu kinakwenda kwa kukishuhida mwenyewe unajua majukumu yapi ya kufanyia kazi."
Aveva alisema: "Mimi ni jemedari mkuu wa Simba hivyo natakiwa kila kitu kiende sawa ndiyo maana nimeamua kuja kukaa huku pamoja na watu wa kazi."
"Ukaribu wangu na wao nitajua mapungufu na ubora uko wapi kwa undani na kutafuta njia ya kusaidiana, kuongeza morali na kuhamasishana katika mambo mbalimbali kwani mchezo huo ni muhimu,"anasema Aveva kwa kujiamini.
"Malengo ya Simba mwaka huu ni kuhakikisha tunachukua ubingwa na mchezo huo na Yanga ndiyo utatoa taswira nzuri kwetu."