CTI: Viroba kufilisi wawekezaji


Vibarua wakikusanya pakiti za plastiki za
Vibarua wakikusanya pakiti za plastiki za kuwekea pombe kali ‘viroba’. Picha na Maktaba 
Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), limesema katazo la pombe kali ndani ya vifungashio vya plastiki maarufu ‘viroba’, litawaathiri wawekezaji  wenye viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo.
Mkurugenzi wa Sera na Ushawishi wa CTI, Hussein Kamote alisema utekelezaji huo unakwenda kinyume na maombi yao waliyoyatoa serikalini ya kupewa muda wa miaka miwili.
Kamote alisema lengo la kuomba muda zaidi, lililenga kufanikisha mchakato wa kuhama teknolojia ya vifungashio vya plastiki na kuingia ya chupa.
Juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba alieleza utaratibu utakaotumika kuondoa sokoni matumizi ya pakiti za plastiki za kufungashia pombe hizo huku akipiga marufuku utengenezaji, usambazaji na uingizaji nchini wa mifuko hiyo.

Related

uchumi na biashara 6390049164930562282

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii