Maige asisitiza kutohusika wizi wa twiga





Maige
Maige 

 Mbunge wa Msalala, mkoani Shinyanga, Ezekiel Maige amewanyooshea kidole wananchi ambao kila wanapomwona humtaka arudishe twiga anaotuhumiwa kuwaiba.
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Bugalama wilayani Kahama juzi, alisema ingawa hakuhusika kuwasafirisha wanyama hao waliopelekwa nje ya nchi, lakini akipita kwenye mikusanyiko watu humpigia kelele wakiimba “Maige rudisha twiga wetu.”
 “Twiga hao hawakuibwa ila walichukuliwa na walibebwa mchana kweupe, huenda ni jambo la kunichafua kisiasa kwa kuwa haiwezekani twiga hao wachukuliwe tangu mwaka 2010 na mwaka 2017 niambiwe niwarudishe,” alisema Maige.
Diwani wa Segese, Johnasani Charles alisema Maige hawezi kukwepa jambo hilo kwa sababu jamii inaamini baada ya suala hilo kufika bungeni, aliondolewa katika nafasi yake ya uwaziri kwa sababu ya wizi wa twiga.



Related

kitaifa 2628315701046838067

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii