P funk - Harmorapa ni Level Nyingine Bana..!!!



Producer mkongwe na mwenye heshima yake P Funk Majani ameibuka na kumzungumzia huku akimsifia msanii anayeibukia kwa kasi katika bongo fleva, Harmorapa na kusema kuwa rapa huyo ni "level nyingine".

Tangu Msanii Harmorapa ameingia kwenye muziki kwa kuanza kujifafanisha na msanii Harmonize, kila wakati rapa huyo amekuwa akiingia kwenye 'headline' mbalimbali na kuzungumziwa na wasanii wengi wakubwa nchini, wengine wakifurahishwa na matendo yake huku wengine wakimdhihaki na kuona kuwa hastaili kuwa mwanamuziki.


Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na picha mbalimbali na Harmorapa mitandaoni zikimuonesha akiwa ameshikilia pesa nyingi jambo ambalo limemfanya producer huyo kuibuka na kumwagia misifa.



Related

michezo na burudani 8700885754269908886

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii