Mbea city yalazimisha sare kwa simba

Timu ya Simba imeendelea kulinda heshima yake baada ya mshambuliaji Shiza Kichuya kuinusuru kufungwa nyumbani kutokana na kuisawazishia kwa mkwaju wa penalti zikiwa zimebaki dakika nne mchezo kumalizika. Simba ilikuwa nyuma kwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City hadi dakika ya 80, lakinikuangushwa kwa Mohammed Hussein 'Tshabalala' katika eneo la hatari kuliifanya Simba kusawazisha kwa mkwaju wa penalti. Kwa matokeo hayo, Simba imelazimika kupoteza pointi mbili katika mbio zake za Ubingwa lakini bado ipo kileleni kwa pointi tatu kutoka ilipo Yanga katika nafasi ya pili. Yanga inacheza na Mtibwa Sugar Jumapili ya Machi 5. Kama Yanga itashinda katika mchezo wake na Mtibwa kwa idadi yoyote ya mabao, itafanikiwa kurudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu na kuishusha Simba kwa tofauti ya mabao. Yanga itakuwa mkoani Morogoro kukabiliana na Mtibwa Sugar katika mchezo unaotajwa kuwa muhimu kwa Yanga hasa kutokana na matokeo ya Simba ya sare ya Simba.

Related

michezo na burudani 540466594340526816

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii