Mipango ya Dr mipango hii hapa

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/mipango-ya-dr-mipango-hii-hapa.html
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mipango ametaja hatua zinazoendelea kutekelezwa na serikali ili kufikia malengo ya uchumi wa Viwanda. Maeneo hayo ni kupambana na rushwa, kuimarisha miundombinu ya umeme na barabara. Dk Mpango amesema pamoja na juhudi hizo, lengo la kufikia uchumi wa Viwanda siyo la serikali pekee. Dk Mpango aliyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa Warsha ya 22 ya tafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Repoa. "Serikali inatengeneza mazingira ya uwekezaji,inatoa fursa kwa kila mtanzania anayehitaji kuwekeza lakini ni muhimu kushirikiana pamoja. Kubadili fikra za watanzania ili wajitokeze zaidi katika fursa hii, "alisema. Warsha hiyo inayofanyika kila mwaka, ina lengo la kujadili changamoto, mbinu, uzoefu na jinsi ya kuimarisha taasisi katika malengo ya uchumi wa viwanda.