mwigulu; aliyemtishia nape bastola sio asikari na mtuhumiwa ameshapatikana.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ameeleza kwa wanahabari kuwa mtu aliyemtishia kwa bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye si askari wa Jeshi la Polisi, lakini ameshapatikana na atashughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa ulinzi na usalama.

Mwigulu alisema hayo baada ya kufungua mkutano wa kazi wa mwaka wa maofisa waandamizi wa polisi, makamanda wa mikoa na wakuu wa vikosi wa Jeshi la Polisi ambao unafanyika mjini hapa.
“Ameshapatikana (kijana aliyemtishia Nape) na atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za ulinzi na usalama ambazo zimekuwa zikifanyika ndani, lakini hazitangazwi,”alisisitiza.

Kijana anayedaiwa kuwa si askari aliyemtolea bastola Nape.

Related

kitaifa 7714897135164703295

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii