Neno kuteleza halina maana Simba’

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/neno-kuteleza-halina-maana-simba.html

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema katika mechi zilizosalia neno ‘kuteleza’ halina nafasi katika kikosi chao.
Simba imeingia Kagera mapema ikiwa na plani B ya kuhakikisha inashinda mechi yake ya Jumapili dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Mayanja alisema: “Tuko Kagera tangu Jumapili, bahati nzuri wachezaji waliokuwa timu ya taifa wameingia leo ‘jana’ na tumefanya nao mazoezi ya pamoja, kiujumla hali ya timu hiko vizuri.
“Hakuna asiyetambua ugumu wa mechi zilizosalia, lakini kama plani yetu ya ushindi huku kanda ya Ziwa itafanikiwa, tutakuwa tumebakiza asilimia ndogo ya kuwa mabingwa.
“Tukifanikiwa kurudi Dar es Salaam na pointi tisa za huku, tutakuwa tumepunguza presha ya ubingwa, tunajua tulichokifuata bila shaka, na tunajua ni mbinu zipi tutatumia ili kushinda mechi hizi tatu za hukua.
“Hata hivyo tunawaombea pia upande wa pili wateleze mechi tatu, tunaamini Mungu atasikia ombi letu na siku si nyingi ndoto ya ubingwa kwa Simba itatimia,” alisema Mayanja.
Kocha huyo raia wa Uganda aliyewahi kuifundisha Kagera Sugar, alisema Simba ya msimu huu inahitaji kuweka rekodi ya tofauti katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kabla ya kutwaa ubingwa.
Mchambuzi, Jeff Leah alisema Kagera Sugar haina cha kupotea katika mchezo huo kama ilivyo kwa Simba itakayoingia kwa presha ya kupata pointi tatu tofauti na itakavyokuwa kwa wenyeji.
“Kagera haiko katika nafasi ya kushuka daraja wala kutwaa ubingwa msimu huu, hivyo itacheza mechi hiyo kwa ‘kurelax’ kwani haina cha kupoteza tofauti na Simba ambayo inahitaji kwa nguvu pointi zote tatu, hivyo wanapaswa kutulia na kucheza mechi hiyo kama mechi nyingine,” alisema Leah.