Njia mbadala za kuzima moto

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/njia-badala-za-kuzima-moto.html
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wametakiwa kuacha tabia ya kuyashambulia magari ya zimamoto kwa madai ya kuchelewa kufika katika tukio la ajali ya moto na badala yake kutumia njia mbadala kukabiliana na moto huo kabla haujaleta madhara makubwa. Akizungumza wakati kikosi hicho mkoa wa Temeke kikitoa mafunzo ya kuzima moto kwa wanafunzi wa sekondari ya Tandika askari wa kikosi hicho Sajini Elvis Mlemba alisema ni muhimu wa wananchi kutoa taarifa mapema pindi moto unapotekea. “Tunapopata taarifa haraka tunajitahidi tufike eneo la tukio lakini utakuwa watu wengine hawaelewi wanawashambulia mmechelewa, tunasisitiza taarifa itolewe huku wakazi wa eneo husika waendelee na jitihada za kuuzima moto”. Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Adam Ali alisema elimu hiyo itamuwezesha kuchukua hatua za awali pindi moto utakapotokea katika mazingira yanayomzunguka.