Rais Magufuli afanya mabadiliko baraza la mawaziri
 
http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/rais-magufuli-afanya-mabadiliko-baraza.html
Rais John Magufuli 
 Rais John Magufuli amefanya mabadiliko madogo  katika Baraza la Mawaziri kwa kumteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Dk Harrison Mwakyembe ambaye anakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyokuwa ikishikiliwa na Nape Nnauye.
Taarifa iliyotolewa leo asubuhi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu,  Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja na wateule wote wataapishwa  kesho mchana.

