RCC kubisha hodi kwa Majaliwa

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/rcc-kubisha-hodi-kwa-majaliwa.html

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Kusudi hilo limefikiwa leo (Alhamisi) wakati wa kikao cha kamati hiyo ambapo imeonekana kuwa miradi mingi iliyopangwa haitatekelezeka kwa sababu halmashauri hazina mapato ya kutosha baada ya Serikali kupitia bajeti ya mwaka 2016/2017 kupitisha kuwa kodi za majengo zikusanywe na Serikali Kuu.
Kufuatia hali hiyo mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amependekeza hoja ya kumuona Waziri Mkuu kwa ajili ya kuzungumza naye kabla ya kuanza kwa Bunge la bajeti ili kuwanusuru na hali hiyo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekiri ukwamo huo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukubaliana na hoja iliyotolewa na mstahiki meya wa jiji ambapo ameahidi kuunda timu ya wataalmu ambayo itawashauri kabla ya kubla ya kwenda kumuona Waziri Mkuu.