Sanchez aiweka Arsenal roho juu

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/sanchez-aiweka-arsenal-roho-juu.html

Kifundo cha mguu cha mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez kimeumia vibaya na inahofiwa kuwa anaweza akawa na madhara zaidi, kwa mujibu wa kocha Arsene Wenger.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile alitolewa zikiwa zimebaki dakika 12 kumalizika kwa mchezo wao wa kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya West Brom juzi.
Sanchez aliumia katika kipindi cha kwanza, wakati alipochezewa vibaya na James McClean.
"Hakutakiwa kucheza kipindi cha pili, lakini alisisitiza kuwa anaweza kuendelea," alisema Wenger. "Lakini mwishowe tuliamua kumtoa."