Mane aipa Liverpool ubingwa Ulaya

   



 Mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane amesema anamatumaini Liverpool itatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa.
Liverpool imefuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo baada ya kuiondoa Porto kwa mabao 5-0 na sasa wanasubili kujua wapinzani wao war obo fainali katika ratiba itakayopagwa kesho.
Mane amekuwa chanzo cha mafanikio ya Liverpool dhidi ya Wareno hao baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa kwanza na kusonga mbele kwa kishindo.
Pamoja na mwaka 2018, kuwa ndiyo mwaka wa kwanza kwa Liverpool kufuzu kwa robo fainali baada ya kuwa nje kwa miaka tisa, Mane anaamini wanaweza kutwaa ubingwa huo.
"Zimebaki klabu kubwa pekee katika hatua hii," Mane aliimbia Sport Bild.
"Tunajua kama unataka kuwa ubingwa ni lazima uwafunge mabingwa. Tuna kiwango cha kuifunga timu yoyote kwa sasa. Tutahakikisha tunatimiza lengo.
"Kwanini Liverpool isiwe juu 2018? Tunataka kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa. Naamini tunauwezo wa kurudia kile kilichofanywa 2005." 

Related

michezo na burudani 5826372335536132097

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii