Simba yatua kwa kishindo Port Said kuivaa Al Masry -VIDEO


 Mabingwa mara 18 wa Ligi Kuu Bara, Simba wamewasili salama jijini Cairo, Misri na kuondoka mara moja kuiwahi Al Masry mjini Port Said.
Simba iliwasili Cairo saa 8 usiku kwa muda wa hapa (saa 9 usiku kwa Tanzania) na kukamilisha taratibu za kuondoka Uwanja wa Ndege wa Cairo saa 9.30 usiku.
Hata hivyo, mabosi wa Simba wakiongozwa na Kaimu Rais, Salim Tryagain walihakikisha msafara unaondoka Cairo muda huo huo, ili kuwahi Port Said yalipo Makao Makuu ya Al Masry umbali wa Km213.
Simba wanaenda katika mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mazoezi yao ya mwisho Dar es Salaam, kocha Pierre Lechantre, alionekana kusisitiza wachezaji wake wapige pasi za haraka ili waweze kupata bao.
Lechatre alikuwa hataki kabisa kuweka mpira nyuma, mara kwa mara alikuwa akiwakomalia mabeki wake Erasti Nyoni na Yusuf Mlipili wasikae na mipira nyuma, badala yake wawaishe mbele.

credity to mwananch media,

Related

michezo na burudani 1197464160636654913

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii