Rashford amtega Mourinho Man United




 Mshambuliaji kinda wa Manchester United, Marcus Rashford anaweza kuondoka Old Trafford ikiwa Jose Mourinho ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo.Taarifa za ndani zimedai mchezaji huyo mwenye miaka 20, haridhishwi na kocha huyo kumuweka benchi katika mashindano mbalimbali.Mourinho amekuwa akimuanzisha benchi mchezaji huyo wa kimataifa wa England tangu alipotwaa mikoba ya Luis Van Gaal.Rashford aliingia akitokea benchi kujaza nafasi ya Alexis Sanchez katika mchezo wa Ligi Kuu England ambao Man United ilishinda mabao 3-2.Kinda huyo anakumbukwa na mashabiki wa Liverpool kwa kufunga mabao yote mawili dhidi ya watani wa jadi Liverpool mwezi uliopita. Man United ilishinda 2-1.Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa mwokozi wa Man United katika mechi ngumu ameanza katika mechi tano kati ya 16 alizocheza msimu huu.Sanchez amezima ndoto ya mchezaji huyo kupata namba kikosi cha kwanza kwa kuwa tayari Mourinho amekuwa akimtumia Romelu Lukaku.Katika mechi 12 tangu Sanchez amejiunga na Man United, Rashford ameanza katika michezo miwili.Mourinho anamtaja kinda huyo ni mchezaji wa aina yake na amemuweka katika rekodi ya washambuliaji watano bora.

Related

michezo na burudani 4797720284844703069

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii