nafasi ya serengeti boys kushiriki fainali za under 17 yazidi kua kubwa





 Huenda tanzania  ikapata  nafasi ya kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 kutokana na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupitisha hukumu.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilikata rufaa CAF kutaka mchezaji wa Congo-Brazzaville, Langa Percy afanyiwe vipimo vya MRI kwa madai kuwa amezidi umri wa miaka 17 jambo ambalo lilipelekea Shirikisho hilo la Afrika kuwapa Congo siku 12 kumpeleka mchezaji huyo mjini Cairo, Misri kwa ajili ya kufanyiwa vipimo hivyo.
Hata hivyo taarifa mpya ambazo mtandao huu limezinasa ni kwamba huenda Congo ikapewa dhamana ya kuandaa mashindano hayo na kupata tiketi ya kufuzu kama mwenyeji huku Serengeti Boys ikipita kwa mgongo huo kwa kuwa Madagascar iliyokuwa iandae michuano hiyo imeonekana kukosa vigezo.
Ofisa Habari wa CAF, Junior Binyam aliliambia mtandao huu kuwa kikao kijacho cha Kamati ya Utendaji ya CAF ndicho kitakachotoa hatma ya mashindano hayo na kusema kama Tanzania imefuzu ama la.
“Sifahamu kama wameshampeleka mchezaji kwa ajili ya kufanyiwa vipimo lakini ninachofahamu ni kwamba Kamati ya Utendaji ya CAF itakapokutana mapema mwezi ujao ndipo itatoa hukumu ya hiyo kesi ili kuona ni nani ana haki ya kufuzu,” alisema Binyam.
Awali, Congo ilishindwa kumpelekea Percy  kwajili ya kufanyiwa vipimo nchini Misri kwa madai yupo katikati ya vita lakini sasa wanalazimika kufanya hivyo kabla ya keshokutwa Alhamisi vinginevyo Serengeti Boys itapewa tiketi hiyo.

Related

michezo na burudani 1395532987908713973

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii