Straika wa Serengeti afuzu Etoile

https://maisharaisi.blogspot.com/2017/01/straika-wa-serengeti-afuzu-etoile.html
Mshambuliaji Yohana Mkomola
Mkomola alijiunga na Etoile kwa majaribio ya siku 15 na atarudi kwa mara nyingine ili kuendelezwa na ataingia mkataba rasmi pale atakapofikisha miaka 18.
Mshambuliaji huyo aliyepata shavu hilo baada ya kufanya vizuri katika mechi tofauti za timu ya taifa ya vijana na Azam aliyokuwa anaichezea alisema, amejifunza mengi kwa kipindi hicho kifupi.
“Kwa siku hizo chache nilizokaa pale, nimejifunza mengi lakini nataka kujifunza zaidi, natarajia kujiunga nao tena,’’ alisema.