Azam, Ndanda kupigwa usiku

https://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/azam-ndanda-kupigwa-usiku.html
Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam itacheza mechi yake ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), dhidi ya Ndanda FC Aprili 5, saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taafira iliyotolewa na TFF inasema robo fainali ya nne ya mashindano hayo itafanyika Aprili 22 kati ya Yanga na Tanzania Prisons FC saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Washindi wa michezo hiyo wataungana na Mbao na Simba zilitangulia hatua ya nusu fainali.
Mbao FC ya Mwanza ilifuzu kwa hatua hiyo baada ya kuitoa Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali ya kwanza uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera Machi 18, mwaka huu.
Simba ya Dar es Salaam imepita baada ya kuishinda Madini FC ya Arusha kwa bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali ya pili uliofanyika Machi 19, 2017 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.