Serengeti Boys wapewa bima




 Mfuko wa Taifa bima ya Afya, NHIF imewatunuku bima wachezaji wa kikosi cha vijana Serengeti Boys ikiwa ni hatua ya kuonyesha wanathamini michezo.
Mkurugenzi wa masoko na utafiti wa kampuni hiyo, Anjela Mziray alisema huu ni mwendelezo wa ushiriki wao katika michezo.
"Tumewapa hiki kidogo kama sehemu ya kuwaunga mkono kwenye hatua ambayo wamepiga kama wawakilishi wa Watanzania wote kwenye mashindano ya vijana," anasema Mziray.
Bima hizo wametunukiwa wachezaji hao zitawafanya kupata matibabu bure bila malipo ya aina yoyote, pindi wapatapo majeraha au kuumwa.

Related

michezo na burudani 5407215112397626374

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii