Stand United yaichapa Transit Camp


 Stand United imeichapa Transit Camp kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Katika mchezo huo, Stand United ilipata bao la kuongoza dakika ya 18, lililofungwa Kheri Mohamed.
Bao hilo liliwachangaya kidogo Transit Camp ambapo walijikuta wakipachikwa lingine la pili katika dakika ya 38, lililofungwa na Sixtus Sabilo.
Kipindi cha pili, Stand United waliendeleza makali yao na kufanikiwa kupata bao la tatu katika dakika ya 76, lililopachikwa wavuni na Mnigeria Abaslim Chidiebele.
Kocha Msaidizi wa Stand United, Athumani Bilali “Bilo”amesema mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi yao ya Ligi Kuu  Jumamosi dhidi ya African Lyon.

Related

michezo na burudani 7280086101866207833

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii