Vijana 1500 waula

https://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/vijana-1500-waula.html
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Kilimo ya Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim amesema leo atawawezesha vijana 1500 kujikwamua na umasikini kupitia kilimo biashara. Biubwa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mpango wa kujikwamua na umasikini kwa vijana kati ya umri wa miaka 18 hadi 30. Akizindua mpango huo alisema ufugaji wa nyuki, samaki pamoja na kilimo cha mboga mboga vitaweza kuwaokoa vijana wengi na hivyo wataepukana na vishawishi vya uvunjifu wa maadili amesema.