Waigizaji wafanye kazi zenye ubunifu.

https://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/waigizaji-wafanye-kazi-zenye-ubunifu.html
Waigizaji wa filamu nchini wametakiwa kuwa wabunifu ili kutengeneza kazi zenye ubora wa kuweza kushindana kwenye soko ndani na kuvuka mipaka pia kwa sababu Kiswahili kinazungumzwa na watu milioni 200 duniani kote. Akizungumza wakati wa utambulisho wa Filamu mpya ya 'Kiumeni' inayotarajiwa kuzinduliwa kesho, katika ukumbi wa sinema wa Century Cinemax Mlimani City, mtayarishaji wa filamu hiyo Ernest Napoleon amesema waigizaji na watayarishaji wanaotengeneza filamu za kiswahili wanapaswa kuwa makini. Filamu ya Kiumeni imewashirikisha mastaa mbalimbali wa filamu nchini akiwemo Irene Paul, Idris Sultan, Antu Mandoza, Mama Abdul na Mhogo Mchungu.