Kuiona Serengeti Gabon bei poa

https://maisharaisi.blogspot.com/2017/05/kuiona-serengeti-gabon-bei-poa.html
Mashabiki wa soka wanaotaka kwenda Gabon kushuhudia mchezo mmoja wa Serengeti Boys hawana budi kujikamua Dola 1172 za Marekani sawa na zaidi ya Sh 2.6 milioni za Tanzania.
Serengeti Boys iko Gabon na Mei 15 itaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa vijana kwa kuwavaa mabingwa watetezi Mali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (Jumatano), Mkurugenzi wa kampuni ya uwakala ya Luhesa Lukaye Sawe amesema kampuni yake kwa kushirikiana na TFF wameingia makubaliano ya kuratibu safari za mashabiki wa Tanzania wanaokwenda Gabon kushuhudia fainali hizo.
"Kwa mtu anayetaka kushuhudia mechi moja atalipa Dola 1172 ambazo zitajumuisha tiketi ndege kwenda na kurudi, hoteli, usafiri wa kwenda na kurudi uwanjani na kiingilio cha uwanjani,"alisema.
Aliongeza kuwa ikiwa shabiki anataka kushuhudia mechi tatu za hatua ya makundi atalipa dola 1770 (sawa na Sh. 4 wakati mashabiki watakaokaa Gabon wakati wote wa mashindano hiyo watalipa Dola 2416 sawa na Sh. 5.5 milioni.
Hatua hiyo inawalazimu mashabiki wa soka nchini kujikamua kama wanataka kuiona Serengeti Boys nchini Gabon.