Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent aendelea kushikiliwa na Polisi






 Jeshi la Polisi mkoa hapa linaendelea kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vicent, Innocent Mosha kutoka na tuhuma za gari lake kuzidisha idadi ya abiria na  kusababisha ajali iliyogharimu maisha ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.
Gari hilo lililopinduka katika eneo la Rotya wilayani Karatu, mkoani Arusha Mei 6, mwaka huu inadaiwa kubeba abiria 38 wakati uwezo wa gari ni kubeba abiria 30.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amesema kuwa wanaendelea kumuhoji mmiliki huyo wakisubiri jalada kutoka ofisi ya mwanasheria wa Serikali ili afikishwe mahakamani.
"Tunaendelea na uchaguzi na faili, likirudi kutoka ofisi ya mwanasheria wa Serikali tutamfikisha mahakamani,"amesema.
Akizungumzia ukaguzi wa magari ya shule, Ilembo amesema kuanzia sasa ukaguzi utakuwa wa kudumu.


Related

kitaifa 8891419631408022164

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii