kesi ya wanafunzi st joseph yazidi kupigwa taree

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/01/kesi-ya-wanafunz-st-joseph-yazidi.html

Mahakama Kuu sasa kufanya usuluhishi katika kesi ya madai ya Sh 6 bilioni iliyofunguliwa na wanafunzi 316 waliokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha St Joseph ambao walirudishwa nyumbani kwa kuwa hawana sifa dhidi ya chuo hicho na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Februari 15,2016.
Usuluhishi huo ulipaswa kufanyika Januari 23, 2017 mbele ya Jaji Rose Temba lakini umesogezwa hadi Februari 15, 2017 kwa ajili ya kusubiri Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutoa muongozo wake.
Katika usuluhishi huo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inawakilishwa na Anna Kalomo ambaye aliomba waziri huyo wa elimu aipitie na atoe muongozo wake ili maamuzi maazuri yaweze kufikiwa.
Kwa upande wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewakilishwa na Rose Rutha, Chuo Kikuu cha St Joseph kimewakilishwa Wakili, Jerome Msemwa huku wanafunzi wakiwakilishwa na wakili, Emmanuel Muga.