Chenge asema hakuna atakayekufa njaa Bariadi




Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge
Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge 
 Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge amewaondoa hofu wananchi jimboni mwake kuwa hakuna atakayefariki dunia kwa njaa kwa sababu vipo vyakula vya kutosha.
Chenge alitoa kauli hiyo katika Kijiji cha Mwantimba Kata ya Matongo mkoani Simiyu baada ya wakazi hao kumwomba awapatie mahindi ya msaada ili kukabiliana na njaa inayowanyemelea.
Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Kija Thelathini alimweleza mbunge huyo kuwa wananchi hulazimika kula mlo mmoja kwa sababu mazao waliyopanda yamekauka.
Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Juliana Mahongo alimtaka mbunge huyo kufikisha kilio chao katika mamlaka husika ili wapelekewe mahindi ya msaada watakayouziwa kwa bei nafu


Related

kitaifa 1834585678457010538

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii