Askofu Mokiwa aendesha misa kuombea Anglikana



Askofu wa Mkuu wa Dayosisi hiyo, Dk Valentino
Askofu wa Mkuu wa Dayosisi hiyo, Dk Valentino Mokiwa. 
 Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam leo limefanya misa maalum ya kuombea amani kanisa hilo ikisimamiwa na Askofu wa Mkuu wa Dayosisi hiyo, Dk Valentino Mokiwa.
Askofu Mokiwa amefanya mahojiano na waandishi wa habari  baada ya misa hiyo leo  Ijumaa na kusema kanisa hilo linaumwa, limeingiliwa na linachafuliwa na mlengwa ni yeye na kazi yake sasa ni kumuomba Mungu atunze kanisa hilo.
"Sijawahi kuuza mali za kanisa mwanaume yeyote aamke aseme nimeuza kipi, sijawahi kufuja mali za kanisa mwenye ushahidi ajitokeze mbele yenu aseme na mwenye ushahidi wa chochote kile ajitokeze, wezi wanajulikana na mimi nawajua," amesema Mokiwa.
Wakati misa hiyo ikiendelea watu wawili waliosemekana wametokea kanisa la Anglikana Magomeni, mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Chesmo na mwanamke mmoja wamekamatwa na jeshi la polisi ndani ya viwanja vya kanisa hilo na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi leo.


Related

kitaifa 8203912336508668755

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii