DC Hapi atoa siku saba kwa ofisa elimu kuhusu walimu





Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amempa siku saba  ofisa elimu wa wilaya hiyo  Fatma Mwiru  kuhakikisha idadi ya walimu katika Shule ya Msingi Kiumbageni iliyopo Kata ya Mbweni inaongezeka.
Ametoa amri hiyo leo Jumanne asubuhi kufuatia wanafunzi wa darasa la kwanza 162 kulazimika  kusoma kwenye darasa moja kwa sababu darasa lingine halina mwalimu.
Amesema haamini kama mrundikano huo wa wanafunzi katika darasa moja unatokea kwenye wilaya yake yenye walimu wa kutosha.
Amefafanua kuwa wilaya hiyo katika baadhi ya shule kuna walimu hawana cha kufanya kutokana na kuwa wengi, hivyo wapunguzwe na kupelekwa kwenye shule hiyo iliyopo Kata ya Mbweni.



Related

kitaifa 6746561965884805764

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii