Serikali yaonya mashabiki wa Simba na Yanga



EMAIL THIS ARTICLE TO A FRIEND

SUBMIT CANCEL




Serikali imetoa onyo kwa mashabiki watakaofanya fujo uwanjani wakati wa mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Mkurugenzi wa michezo wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo amesema mashabiki watakaofanya fujo watachukuliwa hatua na siyo kuziadhibu klabu.
"Tumefunga kamera uwanjani, shabiki atakayefanya fujo ataoneka kwenye kamera atachukuliwa hatua yeye binafsi. Pia mchezo wa kwanza waamuzi walichangia vurugu. Tunatoa rai mpange waamuzi wazuri,"alisema Singo.
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura aliwataka mashabiki kutokwenda uwanjani na matokeo yao.
"Mashabiki msije na matokeo uwanjani, kama mwamuzi ataharibu ataadhibiwa na mamlaka husika," anasema Wambura.   
Naye Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema: "Tunaruhusu mashabiki kuja na jumbe za hamasa, lakini jumbe zinazokashifu viongozi wa serikali na TFF hazitaruhusi na wahusika hatua zitachukuliwa juu yao."
Mkuu wa kitengo cha usalama cha TFF, Ispekta Hashim Abdallah alisema mashabiki watoe ushirikiano, huu ni mchezo mkubwa. Panapotokea changamoto tushirikiane kuzitatua kabla, wakati na baada ya mchezo."        
Ispekta Abdallah alisema "kutakuwa na ulinzi mkali ndani na nje ya uwanja."
Meneja miradi wa Selcon, Galus Runyeta alisema tiketi za mchezo huo zimeshaanza kuuzwa na kufikia sasa tiketi 10000 zimeshauzwa.
"Tiketi zitauzwa hadi Ijumaa hakutakuwa na muda wa nyongeza," amesema
 Viingilio vya mchezo huo kwa viti vya blue ni Sh. 7000, Orange 10,000, VIP B na C Sh. 20,000,  na VIP A Sh30,000.   
Tiketi zinauzwaa Buguruni, Mbagala, Ubunge sheli, Karume, Mtoni kwazizi Ali, na pia kuna mabasi ya Abood yatasafirisha abiria kutoka Morogoro kuja Dar.

Related

michezo na burudani 2965799677735340111

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii