Madiwani wapigwa ‘stop’ kuvaa jeans kwenye vikao
 
http://maisharaisi.blogspot.com/2017/02/madiwani-wapigwa-stop-kuvaa-jeans.html

Madiwani wa Ilala wakiwa katika vikao 
 Madiwani jijini Tanga waliokuwa wakivaa suruali aina ya jeans kwenye vikao vya baraza wanalazimika kuachana na nguo hizo baada ya Meya wa jiji hilo, Mustafa Mhina kupiga marufuku uvaaji wa mavazi hayo.
 Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani jana, Mhina alisema viongozi hao hawaruhusiwi kuvaa suruali hizo  na mavazi mengine ambayo hayana staha.
Mhina amewataka madiwani kuvaa majoho na kofia na kwamba ambao hawatafuata utaratibu huo watatolewa nje ya mkutano.
 Akichangia hoja, Diwani wa Maweni, Joseph Collivas (CCM) aliwataka wajumbe wa Baraza la Madiwani kutoa kero za wananchi ili zipatiwe  ufumbuzi.
