Majaliwa, mshindo wa ziara 40

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/02/majaliwa-mshindo-wa-ziara-40.html

Ziara 40 za Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa tangu ateuliwa, zimemtofautisha na watangulizi wake kutokana na kuwa za kikazi zaidi huku zikiacha vumbi baada ya kuibua madudu na kuwachukuliwa hatua watuhumiwa.
Mwananchi limebaini kati ya ziara 40 alizowahi kuzifanya katika maeneo mbalimbali kwa mwaka mmoja na miezi mitatu tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, zaidi ya asilimia 95 amewachukulia hatua za nidhamu baadhi ya watumishi kutokana na kubaini madudu.
Baada ya kuingia madarakani, Majaliwa aliamuru kukamatwa kwa maofisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.
Watangulizi wake akiwamo Mizengo Pinda na Edward Lowassa walionekana ni watu wa kufanya kazi za kufungua mikutano na kuzindua miradi mbalimbali, lakini Majaliwa ameonyesha tofati katika utendaji kwani katika ziara zake amezifanya zilikuwa mahsusi kuibua madudu au kwenda kusikiliza kero za wananchi.
Mathalani, ziara aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita Babati mkoani Manyara kwenye Kiwanda cha Mbolea Minjingu, aliweka bayana kuwa alikwenda kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea ya Minjingu haikubaliki kwa wakulima.
Alisema alipokuwa kiwandani hapo alikerwa zaidi kukuta mifuko ya kupakia mbolea hiyo, ina anuani ya Nairobi Kenya wakati malighafi inatoka Tanzania.