Wapewa siku saba kusalimisha watoto

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/02/wapewa-siku-saba-kusalimisha-watoto.html

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Mtemi Simoni amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Pendo Malabeja kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti walikopangiwa ndani ya siku saba, vinginevyo wazazi au walezi wao wakamatwe na kushtakiwa mahakamani.
Wanafunzi 474 sawa na asilimia 10 ya wanafunzi 4,749 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika halmashauri hiyo, hawajaripoti.
Akizungumza wakati wa kufunga kikao cha Baraza la Madiwani juzi, Simoni alisema kushindwa kwa wanafunzi hao kuripoti shuleni, wazazi wao wana jambo la kujibu kuhusiana na tatizo hilo.
“Lazima hatua za kisheria zichukuliwe kwa wanafunzi na wazazi ili liwe fundisho kwa wengine,” alisema Simoni.
Awali, akitoa taarifa ya elimu, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji wa Halmashauri hiyo, Peter Misalaba alisema matokeo ya mitihani ya kitaifa wilayani humo hayaridhishi.
Misalaba alisema wanafunzi 4,749 pekee ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, sawa na asilimia 72.7 ya wanafunzi 6,579 waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.