simanzi kwa vyama vyaupinzani congo

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/02/simanzi-kwa-vyama-vyaupinzani-congo.html

Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Etienne Tshisekedi amefariki dunia usiku jana nchini Ubelgiji.
Tshisekedi amefariki akiwa na umri wa miaka 84 alielekea nchini humo kwa matibabu ya kiafya kwa mujibu wa chombo cha habari cha AFP.
Chombo hicho cha habari kiliongeza kuwa hatua hiyo inajiri wakati ambapo chama chake kinaendelea na mazungumzo ya kugawana mamlaka kufuatia hatua ya Rais Laurent Kabila kukataa kujiuzulu baada ya muda wake wa kumalizika kukamilika mwezi uliopita.
Harakati za Tshisekedi kama mwanasiasa wa upinzani zilianza tangu nchi hiyo kujinyakulia uhuru kwani ndiye mmoja wa wachache tu waliothubutu kumkosoa hata Rais Mobutu Sese Seko wakati wa utawala wake uliokuwa umepiga marufuku vyama vya kisiasa vya upinzani.