Umbali wawaongezea wagonjwa maumivu





Wagonjwa wanaofika Hospitali ya Rubya, Wilaya ya Muleba mkoani wanakuwa wamechoka kutokana na kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 60 kutoka vijijijini na ubovu wa barabara, huku wengi wakitumia gharama kubwa kukodi magari au pikipiki, imeelezwa.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na Serikali kwa Hospitali ya Rubya na Zahanati ya Kishuro juzi, Mganga Mkuu wa Rubya, Dk George Kasibante alisema yatasaidia kuwawahisha wagonjwa na wajawazito kwenye hospitali za Rubya, Kagondo na Ndolage au Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera na Bugando mkoani Mwanza.
Diwani wa Viti Maalumu, Fatuma Jawadu alisema wajawazito wanaokwenda kujifungua katika vituo vya afya mbalimbali wilayani hapa, walikuwa wanajifungulia njiani kutokana na kukosa usafiri wa uhakika.
 Fatuma alisema ili kupunguza kero hiyo, halmashauri haina budi kuboresha Kituo cha Afya  Kaigara kinachotumiwa na watu wengi na kwamba, kwa sasa kinajengwa jengo la upasuaji lakini hakina vyoo imara na miundombinu ya maji ni mibovu, hali inayotishia afya ya wagonjwa.
Akipokea magari hayo na kuyabariki kwa niaba ya Askofu wa Jimbo la Bukoba, Mkuu wa Seminari ya Rubya, Padri Marianus Rutagwelera alisema Serikali imetimiza ahadi yake ya kuboresha huduma kwenye hospitali hiyo.
 

Related

maisharaisi 8101892215260141126

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii