BANDARI YA TANGA HATARINI KUTOWEKA



Bandari ya Tanga ipo hatarini kutoweka kama hatua za haraka za kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi zinazoendelea kwa sasa katika Kisiwa cha Toten kinachoendelea kuharibiwa na maji ya bahari, hazitachukuliwa.
Hayo yamesemwa jana na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Donald Ngaile, wakati wa ziara ya Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, alipotembelea Kisiwa cha Toten jana ili kujionea athari za mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kisiwa hicho ndilo eneo ambalo miundombinu ya kuongozea meli zinapoingia katika eneo la Bandari ya Tanga, ilipowekwa na kwamba kumomonyoka kwa kisiwa hicho, kunatishia uhai wa bandari hiyo.
“Kisiwa hicho ndiyo usalama wa bandari ulipo, lakini kasi ya mmonyoko inatishia kwa kiasi kikubwa usalama wa bandari.
“Kwa hiyo, tunaiomba Serikali iangalie hatua za haraka za kunusuru hali hiyo,” alishauri Ngaile.
Kwa upande wake, Kaimu Mhifadhi Mfawidhi wa Hifadhi ya Bandari ya Tanga, January Ndagala, alisema tayari kuna hatua za kuhifadhi kisiwa ambazo wameshaanza kuzichukua.
“Tumejipanga kufanya tathmini ya kina kwa kushirikiana na Jiji la Tanga pamoja na Bandari ili kuweza kuja na namna bora ya kudhibiti mmomonyoko wa ardhi kisiwani hapo,” alisema Ndagala.

Related

kitaifa 1699158822986684181

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii