Lissu kizimbani, asomewa mashtaka matano


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesomewa mashtaka matano na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi  likiwamo ya kutoa maneno  yenye nia ya kuhimiza hisia za kidini ambayo yangeweza kupelekea uhasama baina ya jamii za Watanzania.
Lissu amekana mashtaka yote na upande wa mashtaka umedai upelelezi umekamilika na wameomba wamsomee maelezo ya awali leo (Ijumaa).
Lissu  ambaye anajiwakilisha yeye mwenyewe mahakamani hapo aliomba maelezo hayo ya awali yasomwe Jumatatu, ili aweze kuhudhuria uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) unaotarajia kufanyika kesho.
Ameomba apewe dhamana kwa masharti nafuu

Related

siasa 705059518292674810

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii