Meya wa Ubungo kumpeleka Makonda kortini





Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob

Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema Jumanne wiki ijayo  atafungua kesi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na  madai ya kuwa na vyeti feki.
Jacob pia amesema, atamshtaki Makonda katika sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma, tume ya haki za binadamu pamoja na utawala bora.
Amesema kesi hiyo ambayo itaongozwa na mawakili Tundu Lissu pamoja na Peter Kibatara.
“Tunachosubiri ni wanasheria wamalize mchakato wa uchaguzi Chama cha Wanasheria Tanganyika (TSL) na mara watakaporejea kutoka Arusha tutakwenda mahakamani” amesema  Jacob.


Related

kitaifa 555778647186230294

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii