Magendo tanga yashika kasi

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na vyombo vingine vya ulinzi wamekamata shehena ya bidhaa za magendo katika Bandari Bubu ya Kigombe zenye thamani ya zaidi ya Sh73 milioni. Akizungumza kwenye ghala la kuhifadhia mali bandarini, Menaja wa TRA Mkoa wa Tanga, Swalehe Byarugaba alisema shehena hiyo ni mchele, sukari, madumu ya mafuta na viberiti kutoka nje vyenye thamani zaidi ya milioni 73. Byarugaba alisema wamekuwa wakifanya doria hasa usiku katika Bandari Bubu ya Kigombe na sehemu nyingine ambazo wamekuwa wakipokea taarifa za ushushaji mali za magendo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema wamekuwa wakifanya doria usiku na mchana bandarini na mpaka wa Horohoro. Wakulyamba alisema kuna baadhi ya washukiwa wa mali za magendo wamehojiwa na kutoa onyo kwa wasafirishaji wa bidhaa kwa njia za panya.

Related

kitaifa 6672145482467001148

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii