Magufuli katengua tena

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Dk Crispin Mpemba kuanzia Machi 4 kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwamo mikataba ambayo shirika hilo liliingia. Baada ya kuondolewa katika nafasi hiyo, Dk Mpemba atachunguzwa dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Rebecca Kwandu imesema Waziri wa Nchi, Tamisemi, George Simbachawene aliunda timu kufanya uchunguzi wa madai hayo na matokeo yalionyesha kuwapo kwa hoja zinazohitaji uchunguzi. “Uamuzi umechukuliwa kwa kuwa tuhuma za awali zilizojitokeza dhidi yake zinajenga hoja ya kuhitajika kufanyika uchunguzi zaidi,” inasema taarifa hiyo ikimnukuu Simbachawene. Mwaka jana, waziri huyo alifanya ziara katika shirika hilo na kusikiliza kero za wafanyakazi mbalimbali, ikiwamo kutopanda vyeo na madaraja na kutolipwa malipo ya muda wa ziada. Shirika la Elimu Kibaha lilianzishwa mwaka 1963 likiwa na majukumu ya kusimamia sekta za elimu, afya, sheria na nyinginezo katika Mkoa wa Pwani.

Related

kitaifa 1121240921371650640

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii