Man United yamtaka Kane

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/man-united-yamtaka-kane.html

Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane
United itajaribu kumchukua mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane, 23, kama itachemsha katika mbio za kumnasa nyota wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann (25).
United imetega jicho lake kwa Kane ambaye msimu uliopita aliibuka kuwa mfungaji bora Ligi Kuu ya England akimaliza na mabao 25 na tayari msimu huu ametupia mabao 17 akiongoza katika chati sambamba na Alexis Sanchez na Romelu Lukaku.
Mshambuliaji Wayne Rooney anatazamiwa kuondoka katika dirisha kubwa la majira ya joto mwaka huu na tayari United imeanza kazi ya kutafuta mrithi wake kwa sasa kwa ajili ya kusaidiana na Zlatan Ibrahimovic ambaye ataongezewa mkataba.