Moto wazua taaruki aicc

 Wajumbe wa Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF  wamelazimika kusitisha mkutano huo  leo baada ya kuzuka kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme. Hitilafu hiyo inadaiwa kusababishwa na moja ya taa katika ukumbi wa Simba AICC kupiga shoti na kusababisha mfumo mzima wa umeme kukorofisha. Hali hiyo imesababisha wajumbe hao kusitisha mkutano wao ili kupisha mafundi kurekebisha hitilafu hiyo ambapo walifanikiwa kutengeneza. Hata hivyo, moto huo haukusababisha madhara yoyote ya kibinadamu na tayari tatizo hilo limerekebishwa ambapo wajumbe wamerejea kuendelea na mkutano huo. 

Related

kitaifa 185438225544544544

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii