Shehena ya viroba yakamatwa Temeke
 
http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/shehena-ya-viroba-yakamatwa-temeke.html
  Shehena ya viroba imekamatwa leo (Alhamisi) katika kiwanda cha Global Ltd kilichopo Temeke, wakati wa operasheni ya kukamata vinywaji vilivyofungashwa kwenye pakiti  maarufu viroba inayoendelea jijini hapa.
Polisi walilazimika kuingia kwa nguvu na kukuta katoni 12,000 za viroba kwenye kiwanda hicho.    
 Mkuu wa operasheni hiyo,  Inspekta Aron Nzala amesema viroba hivyo lazima viharibiwe.

