Soko la bilioni moja kujengwa Kinondoni

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/soko-la-bilioni-moja-kujengwa-kinondoni.html
Halmashauri ya Manispaaa ya Kinondoni imesema itajenga soko kubwa litakalogharimu Sh 1bilioni katika eneo la Magomeni. Akizungumza jijini leo (Alhamisi) katika kikao cha baraza la madiwani, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta alisema kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kutengwa kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018. Alisema makadirio ya bajeti ya Halmashauri hiyo ambayo ilipitishwa na madiwani ni Sh 160bilioni.