Sturridge njiani kuelekea psg

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/sturridge-njiani-kuelekea-psg.html
Mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain wanajiandaa kutoa ofa ya kumchukua mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge. PSG wana nafasi ya kumpata kwa sababu Liverpool inafikiria kuachana na nyota huyo wa kimataifa wa England. Sturridge amepungukiwa na makali yake katika utawala wa kocha, Jurgen Klopp huku akiwa amecheza mechi 14 tu za Ligi Kuu msimu huu na klopp amekuwa aiwatumia zaidi mastaa wake, Sadio Mane, Adam Lallana, Roberto Firmino na Adam Lallana. Inasemekana kuwa Tottenham na Arsenal pia zinaweza kumuwinda staa huyo wa zamani wa Manchester City na Chelsea na dau lake linaweza kuwa juu ya pauni 25 milioni wakati huu Klopp akiwinda mshambuliaji mpya.