Suarez ampongeza messi

Luis Suarez anaamini Lionel Messi ni mchezaji bora wa wakati wote. Mshambuliaji huyo ameyasema hayo wakati akielezea uamuzi wake wa kukataa kujiunga na Real Madrid. Suarez ameungana na Messi Camp Nou mwaka 2014 akiwa pamoja na Neymar. Watatu hao inaaminika wametengeneza safu bora ya ushambuliaji duniani kwa sasa wanayoiita, MSN. Nyota huyo wa Uruguay amesema hana wasiwasi kuhusu ubora wa Messi duniani akisema ni mshambuliaji wa kipekee. "Messi ni bora katika historia ya soka," Suarez ameimbia Onda Cero. Messi amefunga mabao 21 na Suarez (20) wakiongoza katika orodha ya ufungaji na kuisaidia Barcelona kukalia usukani wa La Liga wakiwa mbele kwa pointi moja zaidi ya Madrid yenye mchezo mmoja mkononi.

Related

michezo na burudani 1687201481624529936

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii