Kimpoulsen atoa wito serenget kuungwa mkono

Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Soka cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Kim Poulsen ametoa tathimini ya mwelekeo wa timu ya vijana itakayoshiriki fainali za vijana za Afrika za Mwaka 2019. Tanzania itaandaa fainali za chini ya miaka 17 kwa mara ya kwanza mwaka 2019. Poulsen amesema msingi wa Serengeti ya 2019 utajengwa na vijana wanaoandaliwa na TFF kupitia programu mbalimbali. "Tulikuwa na kambi hapa TFF, vijana 20 wa chini ya miaka 15 wamefanya vizuri na tunakusudia kuwajumuisha kwenye kikosi cha wachezaji waliopo Mwanza." "Tunapojiandaa kwa fainali za Afcon lazima tujue tuna jukumu lingine 2019, ambalo linahitaji maandalizi. Msingi wa hawa vijana ni juhudi za TFF, lakini zinatakiwa kuungwa mkono na wadau wote," alisema kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars. Aidha Poulsen alisema Watanzania wote wanatakiwa kuhamasika kuisapoti timu ya taifa ili timu hiyo ifanye vizuri katika fainali hizo. Tayari serikali ilishatangaza kamati ya watu 10 inayoongozwa na mwanahabari mkongwe Charles Hillary kwa ajili ya kutoa hamasa kwa Watanzania. Katika hatua nyingine Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kesho Serengeti Boys itakwenda Bagamoyo kutembelea kituo cha vijana walioathirika na dawa za kulevya. "Vijana hawa (wa Serengeti Boys) wako kwenye umri ambao una changamoto hivyo hii itakuwa fursa yao kujionea hatari za dawa za kulevya,"alisema Lucas.

Related

michezo na burudani 837306571899381301

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii