Uwekezaji sababu ya utenguzi katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu.

Rais John Magufuli ametengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Uledi Mussa mjini Dodoma hapo jana . Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema hatua ya utenguzi huo ni kutokana na kutozingatiwa kwa taratibu zinazotakiwa katika kushughulikia masuala ya uwekezaji. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa utenguzi huo pia umefanyika ili kupisha uchunguzi wa ukiukwaji huo wa taratibu za uwekezaji.

Related

siasa 7371161291589243296

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii